Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia mwanamke anayefahamika kwa jina la Marusi Samweli kwa tuhuma za kumjeruhi mpenzi wake kwenye uume kwa kumkata na wembe.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia tarehe 10 Januari, 2020 katika nyumba moja ya kulala wageni ya Gibita iliyopo Mugumu wilayani Serengeti.
Akizungumza kwa shida akiwa chini ya uangalizi wa waganga hospitali ya Nyerere akipata matibabu aliyejulikana kwa jina la Joseph amesema alikatwa na mhudumu wa nyumba hiyo baada ya kushindwa kumlipa Sh15,000 badala ya Sh20,000 walizokubaliana kulipana na kwa kila mshindo mmoja ni Sh5,000 na yeye alipiga nne na kutoa fedha pungufu.
"Kwanza tulianza kwa vinywaji kisha tukakubaliana kila (hatua) Sh5,000 lakini akaomba kwanza Sh20,000 nikalipa, tumelala kila baada ya (hatua) nilikuwa nalipa Sh5,000 mitatu nililipa huu wa nne sikulipa akanidai nikamwambia akate kwenye Sh20,000 ya kwanza akagoma.”
“Tukalala alfajiri wakati naaga niwahi kijijini kwenye kazi za uchimbaji dhahabu, kumbe alikuwa na wembe ghafla akashika sehemu yangu ya siri na kukata kuanzia chini kwenye sehemu ili akate kabisa nikapambana lakini akawa ameishaniumiza vibaya," amesema mwanaume huyo.
Amesema akapiga kelele watu wakajitokeza kumsaidia na kutoa taarifa polisi waliofika na kuwachukua wote na mhudumu huyo.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo, Tanu Warioba amesema ataongea baada ya kumaliza kumhudumia majeruhi huyo.
Katika tukio lingine, Juma Waryoba maarufu kama (Kisangura) 27, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kisu mara kadhaa mwilini kwake.
Kamanda Shillah ameongeza kuwa tukio hilo limetokea wilayani Butiama ambapo mwanaume huyo anatuhumiwa kumuua mke wake kwa kuchoma na kisu na kisha kutoroka kusikojulikana huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda ametoa wito kwa wananchi wa mko wa Mara kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kama kuna migogoro ndani ya familia ni vizuri kuitatua kwa njia ya mazungumzo na sio kutumia nguvu, akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya Jamuuri ya Muungano wa Tanzania.