Shirika la Afya UIimwenguni - WHO limetangaza mlipuko wa virusi vipya vya corona nchini China ambavyo vimesambaa katika nchi nyingine kadhaa kuwa hali ya dharura ya kimataifa.
Hii ni baada ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo kusambaa kwa kasi katika kipindi cha wiki moja, ikiwemo idadi ya vifo vya watu 24 viliyotokea katika saa 24 leo Ijumaa.
China imeripoti wagonjwa 9,692 waliothibitishwa kuambukizwa huku idadi ya vifo ikifikia 214. Nyingi ya visa hivyo vimeripotiwa katika mkoa wa Hubei na mji mkuu wake Wuhan, ambao ndio kitovu cha mlipuko huo.
Hakuna vifo vilivyoripotiwa nje ya China. Akizungumza na wanahabari mjini Geneva, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ametaja hofu iliyopo ya kusambaa kwa virusi hivyo miongoni mwa watu nje ya China.
Amesema tangazo hilo la hali ya dharura sio la kura ya kutokuwa na imani na China. Badala yake, WHO inaendelea kuwa na imani na uwezo wa China kuudhibiti mripuko huo.
Social Plugin