Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kikundi Cha Kwaya Ya Bunge kimeaanza Rasmi Kuongoza Kuimba Wimbo Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki Na Wimbo Wa Taifa Pindi Shughuli Za Bunge Zinapoanza.
Awali, wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi na ufungaji wa mikutano ya Bunge ulikuwa ukiimbwa na kwaya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini leo uliimbwa na watumishi wa Bunge.
Akizungumza leo Jan,28,2020, bungeni jijini Dodoma Spika Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia sasa bunge ameliamuru kuwa na desturi ya kuimba nyimbo hizo muhimu pindi vikao na shughuli za bunge zinapoanza .
Ndugai amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwafundisha watumishi hao ambapo baada ya kuimba wabunge waliwapigia makofi kuwapongeza.
___________________
WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
1. Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
Chorus
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.