Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZITTO KABWE AMJIBU SPIKA NDUGAI


Mbunge Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amemjibu  Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyehoji sababu za yeye kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka Tanzania inyimwe mkopo wa elimu.


Ndugai ametoa kauli hiyo leo Ijumaa   bungeni ambapo amesema  Zitto kuandika barua hiyo ni tofauti  za kisera, lakini kuzuia fedha za Benki ya Dunia ni kwenda mbali zaidi na haimsaidii chochote zaidi ya kuwakomoa wananchi Wanyonge.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Zitto ambaye yupo nchini Uingereza amesema, “hakuna tofauti ya kisera katika suala la watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Ilani ya CCM iliahidi hilo, wananchi mwaka 2015, vyama vya Upinzani viliahidi hilo na wananchi 2/3 wanaunga mkono hilo.”


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com