Ebenezer Television ni kituo kipya cha habari ambacho kinatarajia kuanza kurusha matangazo yake kutokea Mikocheni Dar es Salaam. Kituo kinahitaji wafanyakazi katika Nyanja zifauatazo;
1. Mhariri Mkuu – Nafasi moja (1)
- Awe na Shahada ya Uandishi wa Habari au Mawasiliano ya umma
- Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu katika nafasi hiyo
- Awe amelelewa katika maadili ya kikristo.
- Awe na uwezo wa kusimamia uzalishaji wa vipindi
- Awe amehitimu katika vyuo vikuu vinavyotambulika na serikali.
2. Wazalishaji vipindi – Nafasi tatu (3)
- Awe ana kiwango cha chini cha Stashahada kutoka Chuo kinachotambulika.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika nafasi hiyo
3. Waandishi wa Habari – Nafasi tatu (3)
- Awe ana kiwango cha chini cha Stashahada kutoka Chuo kinachotambulika.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika nafasi hiyo
4. Wahariri wa picha nyongefu na wasanifu – Nafasi mbili (2)
- Awe na Stashahada kwenye uandishi wa habari, uhariri picha au ubunifu wa matangazo.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili.
5. Wapiga picha nyongefu – Nafasi nne (3)
- Wawe na elimu kuanzia Astashahada katika upigaji picha nyongefu
- Awe na ujuzi wa sauti za picha nyongefu
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili.
6. Warusha Matangazo – Nafasi tatu (3)
- Awe na Stashahada katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
- Au Stashahada katika teknolojia ya mawasilianao na elektroniki
- Awe na uwezo wa kutatua matatizo ya kiufundi
- Awe na uwezo wa kushauri vifaa bora kutokana na teknolojia
7. Wasoma Habari – Nafasi tatu (3)
- Awe na elimu isiyo chini ya Astashahada ya Uandishi wa Habari au sifa inayofanana na hiyo.
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika fani husika
8. Mkutubi – Nafasi moja (1)
- Awe na elimu isiyo chini ya Astashahada ya utunzaji kumbu kumbu
- Awe ana ujuzi wa kutunza vielelezo vya sauti na picha nyongefu
- Uzoefu wa zaidi ya mwaka mmoja.
9. Msimamizi wa vipindi – Nafasi moja (1)
- Awe na elimu isiyopungua astashahada ya uandaaji na usimamizi wa vipindi
- Awe anajua kupanga ratiba za vipindi katika kituo cha runinga.
- Awe anajua kupanga utaratibu wa matukio ya kitaifa au kikanisa yatakayotokea.
- Awe anajua kupanga na kuratibu matangazo ya biashara katikati ya vipindi pale endapo tangazo litakuja.
10. Mratibu wa maudhui mtandaoni – Nafasi moja (1)
- Awe na elimu isiyopungua Astashahada
- Awe na uzoefu wa mitandao ya kijamii
- Mwenye ujuzi wa mifumo ya kielectronika na komputa
11. Msimamizi wa Utawala – Nafasi moja (1)
- Awe na elimu ya shahada ya awali katika Uongozi yaani (Public Administration, Leadership and Governance.
- Mwenye ujuzi wa habari na Mawasiliano atapewa kipaumbele
- Awe amelelewa katika maadili ya dini ya KIKRISTO
- Awe tayari kufanya kazi nyingine zinazoendana na nafasi hyo
- Awe na uwezo wa kufanya tathmini ya wafanyakazi waliopo na kushauri Uongozi njia bora ya kuboresha.
- Uzoefu wa miaka miwili katika nafasi kama hyo
12. Mhasibu – Nafasi moja (1)
- Awe na elimu ya shahada ya awali katika masuala ya fedha
- Awe amelelewa katika maadili ya kikristo
- Awe na uelewa katika masoko na biashara
- Awe na uzoefu wa miaka miwili
- Awe amelelewa katika maadili ya KIKRISTO
13. Fundi sanifu wa umeme – Nafasi moja (1)
- Awe na stashahada ya umeme katika chuo kinachotambulika
- Awe na uzoefu wa vifaa vya electronics na sauti
- Awe anaufahamu umeme wa phase moja na phase tatu
- Awe na uwezo wa kufuatilia tatizo la umeme na kulitatua
- Awe na ujuzi wa kuunganisha na kuwasha generator.
B. NAFASI ZA WAKURUFUNZI (INTERNS)
1. Waandishi wa Habari – Nafasi tatu (3)
2. Mhariri wa picha – Nafasi mbili (2)
3. Msaidizi wa msimamizi wa vipindi – Nafasi mbili (1)
4. Mrusha Matangazo – Nafasi mbili (2)
5. Wapiga picha – Nafasi mbili (2)
6. Wakutubi – Nafasi mbili (1)
7. Waandaaji vipindi – Nafasi mbili (2)
- Wawe na ujuzi katika fani husika uzoefu si lazima AU awe mwanafunzi anayetarajia kumaliza masomo katika fani husika
C. Watendaji wa kujitolea (Volunteers)
1. Wapiga picha – Nafasi 1
2. Wahariri picha – Nafasi 3
3. Waandaaji vipindi – Nafasi 4
4. Afisa Masoko – Nafasi 3
Maombi yote yaliyo ambatanishwa na nakala za vyeti na CV yatumwe kwa;
Mratibu wa Mradi - Ebenezer Television
S.L.P 4067
Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
AU
Kwa barua pepe ebztvtz@gmail.com katika mfumo wa PDF na viambatanisho vyote viwe katika nakala moja. Mwisho wa kutuma maombi ni February 12, 2020.
Social Plugin