Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATIWA MBARONI AKIIBA SADAKA KANISANI


Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Peter Muiya Irungu anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuiba sadaka katika Kanisa Kuu la James lililopo Murang’a nchini Kenya.


Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo hujifanya anasali na watu wote wanapoondoka Kanisani, anafungua masanduku ya sadaka kwa kutumia waya maalum.

Uongozi wa Kanisa hilo uliamua kuweka kamera za siri baada ya sadaka kuanza kupotea, kanisa hilo limesema limeshangazwa na kitendo hicho cha Irungu, kwakuwa ni mmoja kati ya waumini wenye mahudhurio mazuri Kanisani na hajawahi kukosa ibada hata siku moja.

Aidha, watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyo wanasema alianza tabia za wizi tangu mwaka 2018.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com