Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera amehukumiwa kulipa faini Sh100 milioni baada kukiri kosa la utakatishaji fedha na pia kulipa faini ya Sh250,000 au kwenda jela miezi mitatu kwa kukiri kukwepa kodi,pamoja na fidia ya shilingi milioni 172.
Mapema leo, Kabendera aliyekuwa akikabiliwa na makosa matatu, alifutiwa kosa lake alilokuwa akidaiwa Kuongoza Genge la Uhalifu.
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota korokoroni tangu alipofikishwa mahakamani hapo Agosti 5, 2019.
Kabendera anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.Mil 173 ndani ya miezi 6, huku kiasi cha Sh.Mil 100 akiwa tayari ameshaingiza katika akaunti ya Serikali.
Kabendera kwa sasa yupo huru, huku akitakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Social Plugin