Madiwani 11 wa Chadema Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiwemo Meya wa Jiji hilo wamejiuzulu na kuhamia CCM leo Jumatatu Februari 24, 2020.
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.
Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.
Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
Social Plugin