Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema wamemkamata Mtume Boniface Mwamposa Jijini Dar es salaam alipokuwa amekimbilia baada ya kutoroka mkoani Kilimanjaro kutokana na tukio waumini wake kugombea kukanyaga mafuta ya upako na kusababisha vifo vya watu 20.
Simbachawene ametoa pole kwa Familia ya Watu 20 waliopoteza maisha wakati wakitoka katika ibada hiyo Mjini Moshi.
Amesema Wizara itaweka Kanuni na Taratibu kali za Usajili wa Taasisi zinazotoa Huduma za Maombezi(Ministries) ambazo baadhi zinavunja Sheria.
Social Plugin