BRELA YAJIDHATITI UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WADAU WAKE


Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA akiwa katika kikao cha kwanza na wafanyakazi tangu ateuliwe kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.
**
Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka mikakati mizuri katika kuhakikisha kwamba wadau wake wanapata huduma yenye ubora.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Nyaisa amewataka wafayakazi kufanya kazi kwa bidii na kila mmoja kuwa tayari kusikiliza na kumsaidia mteja punde anapokutana naye.

“BRELA ni Taasisi ya Umma na msingi wake ni kutoa huduma kwa Watanzania wote katika hali ya haki na Usawa bila kujali tofauti za dini, kabila au siasa”, alisema Bw. Nyaisa.

Akizungumzia kuhusu maoni ya wadau kuhusu changamoto ya mfumo, Bw. Nyaisa amebainisha kwamba tayari suala la mfumo linafanyiwa kazi na punde suala hilo litabaki kuwa historia.

“Changamoto ya mfumo wa usajili imezungumzwa na wadau wengi, hivi sasa mfumo wa usajili unafanyiwa maboresho makubwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za BRELA kwa njia ya mtandao.

Sambamba na hilo uelewa kwa wadau wengi juu ya matumizi ya mfumo huu bado upo chini, hivyo jitihada za ziada zimefanyika kuandaa kituo cha miito ya simu mahususi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wadau wetu kwa ukaribu zaidi”.Alibainisha Bw. Nyaisa.

Aidha Bw. Nyaisa ametoa wito kwa wadau BRELA kuendelea kuhuisha taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa mtandao wakati changamoto wanazokutana nazo zikiendelea kufanyiwa kazi.
Wafanyakazi wa BRELA wakifuatilia kwa umakini maelekezo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Godfrey Nyaisa (hayupo pichani) katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano BRELA Ofisi Kuu, Jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post