Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amesoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kwa kipindi cha kuanzia Januari 2016 hadi Desemba 2019 kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoani humo na kueleza kuwa ilani hiyo ya uchaguzi imetekelezwa kwa vitendo.
Telack amesoma taarifa hiyo leo Februari 21, 2020 wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga kilichokuwa na lengo la kusoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala Mlolwa.
Telack amesema Ilani hiyo ya Uchaguzi imetekelezwa kwa asilimia kubwa, ambapo wananchi wametekelezewa miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo Sekta ya Afya, elimu, madini, maji, umeme, ardhi, barabara, pamoja viwanda.
“Ndugu wajumbe utekelezaji huu wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, imetekelewa kwa asilimia kubwa ambapo mwenye macho haambiwi tazama, nadhani kila mtu anajionea maendeleo yaliyopo katika mkoa wetu wa Shinyanga,”amesema Telack.
“Tukizungumzia kwenye sekta ya viwanda katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019, Mkoa umejenga viwanda 189 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kuanzisha viwanda vipya, Utekelezaji huu ni sawa na asilimia 89 zaidi ya lengo la kuanzisha viwanda 100, na juhudi za kuhamasisha jamii kuanzisha viwanda vipya katika mkoa zinaendelea kufanyika", ameongeza.
Pia amesema katika utoaji wa huduma ya maji vijijini unaofanywa na Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA), utoaji wa huduma ya maji vijijini umeongezeka kutoka asilimia 51.0 mwaka 2015 hadi asilimia 54.45 mwaka 2019.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amewataka wajumbe wa kikao hicho wakayazungumze kwa wananchi yale ambayo yamesomwa kwenye taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi, ili wajue namna CCM ilivyochapa kazi kuwaletea maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Thomas Ntegwa, ambaye aliongoza toka mwaka 1965 hadi 1977, amepongeza juhudi zinazofanywa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa wananchi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kipindi cha kuanzia Januari 2016- Desemba 2019, kwa kutumia Projector leo wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Thomas Ntegwa, akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga na kupongeza namna ilani ya uchaguzi ya CCM ilivyotekelezwa kwa wananchi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela, akipongeza namna ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ilivyotekelezwa kwa wananchi.
Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige akizungumza kwenye kikao hicho.
Mbunge wa viti maalum Azza Hilal Hamad (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje, akifuatiwa na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Ernestina Richard, na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela, wakiwa kwenye kikao.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga TaLaba, wakwanza kulia ,akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha kwenye kikao.
Mwenyekiti wa kwanza CCM Mkoa wa Shinyanga Thomas Ntengwa wa kwanza kulia, akifuatiwa na Mbunge wa Ushetu Elias Kwandikwa, ambaye ni Naibu wa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Social Plugin