Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM YAVUNA MADIWANI WATANO WA ACT WAZALENDO


Madiwani  watano wa chama cha ACT Wazalendo mkoani Kigoma wametangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Walitangaza uamuzi huo jana katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.

Walisema wamechukua uamuzi huo kwa kujiuzulu nafasi zao za udiwani na nafasi zote za uongozi ndani ya ACT Wazalendo na kujinga na CCM kuanzia jana.

Madiwani hao ni Hamis Rashid (Kata ya Gungu), Amduni Nassor (Kata ya Kasingirima), Fuad Sefu (Kata ya Kasimbu), Ismail Hussein (Kata ya Kagera) na Mussa Ngogolwa (Kata ya Kipampa), wote kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akiwapokea madiwani hao, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally alisema anafurahi kwa kuwa kila wanapopata mwanachama mpya uwezo wa chama katika kupambana na kuendelea kuongoza nchi na Serikali zake mbili unaongezeka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com