CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MKOA WA SHINYANGA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA.
YAH: KUFUKUZWA UANACHAMA NDUGU CHARLES SHIGINO.
Baraza la Uongozi Mkoa Shinyanga, katika kikao chake cha dharula kilichoketi Tarehe 11.02.2020, kimeamua kumfukuza uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu Charles Shigino, aliekuwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Kwa Mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006, Toleo la 2016. Ibara ya 5.4. Inaeleza juu ya “Kukoma kwa Uanachama.” Kwamba, Ibara 5.4. (1 , 2, na 3) inaeleza kuwa; Mwanachama atakoma uanachama wake kwa kujiuzulu , kufariki , kuachishwa ama kufukuzwa.
Kwa mantiki hiyo, Ndugu Charles Shigino, amefukuzwa Uanachama wa CHADEMA, kutokana na kupatikana na makosa ya utovu wa nidhamu na usaliti kwa Chama pamoja na kwenda kinyume cha Katiba ya Chama, Kanuni na Maadili ya Viongozi wa Chama, na hivyo; anakosa sifa ya kuwa Mwanachama wa CHADEMA kwa mujibu wa Ibara ya 5.4.5 ya Katiba ya Chama.
Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa Umma na Wanachama kuwa Ndugu Charles Shigino, kuanzia tarehe 11.02.2020, si Mwanachama wa CHADEMA tena.
Imetolewa na;
EMMANUEL NTOBI
MWENYEKITI (M)SHINYANGA
13.02.2020
Social Plugin