Mechi kati ya Chelsea na Bayern Munich iliwashuhudia wababe wa Bundesliga wakipiga hatua kubwa ya kukaribia kufuzu kwa duru ya nane bora ya Ligi ya Mabinwa baada ya kushinda 3-0 uwanjani Stamford Bridge.
Matokeo ya kuridhisha katika awamu ya pili siku ya Jumanne, Februari 25 usiku, yalichochewa na Robert Lewandowski ambaye alisadia Bayern kutwaa ushindi.
Upande zote zilionyesha umahiri katika awamu ya kwanza na kutoka sare tasa kuelekea muda wa mapumziko, huku Thomas Muller akikaribia kuvunja kimya baada ya kupiga shuti iliyotua juu ya lango.
Lewandowski pia alinyimwa nafasi mara mbili na Willy Caballero kufunga bao, huku juhudi za Marcos Alonso dakika ya 41 ikizua hatari kwa Chelsea.
Katika kipindi cha pili, wenyeji walionyesha ari ya kuwa kifua mbele huku Manuel Neur akilazimika kupangua mikiki ya Mason Mount na Ross Barkley.
Hata hivyo, Bavarians walifunga bao la kwanza kupitia kwa Serge Gnabry ambaye alivurumisha kombora lililotua kimyani baada ya kuwasiliana na Lewandowski.
Gnabry alisawazisha bao hilo dakika tatu baadaye kufuatia usaidizi wa Lewandowski, kabla ya fowadi huyo kuingia katIka orodha ya watingaji bao dakika ya 76 na kuzima ndoto ya Chelsea.
Matumaini ya wenyeji kupata bao la kufutia machozi ilididimia kunako dakika ya 84 baada ya Alonso kutimuliwa uwanjani kwa kumuangusha Lewandowski.
Masogora wa Frank Lampard kwa sasa wana kibarua kigumu cha kubatilisha matoke hayo wakati wa ziara yao ya Ujerumani kwa mechi ya marudiano ili kufuzu kwa raundi nyingine ya kivumbi hicho cha Uropa.