Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DC BABATI APIGA MARUFUKU MICHEZO YA KUBAHATISHA MAENEO YA VIJIJINI

Na John Walter-Babati.

Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu, amepiga marufuku michezo ya kubahatisha (BONANZA)  katika maeneo ya Vijijini na kuagiza waziondoe zote zilizopo.

Amesema kwa vijijini hakuna sifa ya kuwepo kwa michezo hiyo hivyo waipeleke kwenye kumbi za starehe maeneo ya Mijini.

Mkuu wa wilaya Bi. Kitundu amechukua maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, kwamba michezo hiyo haisaidii chochote katika maeneo yao zaidi ya kuwapotezea muda vijana.

"Ni kweli hawajakiuka masharti, lakini bado ofisi yangu  inasema hawa watu wa Bonanza wananchi wanawakataa na sijui kama kwenye vijiji vyetu kuna sifa ya kuwekwa mashine hizo, sasa kauli ya mkuu wa wilaya ni kwamba katika halmashauri ya wilaya ya Babati na mkurugenzi ambaye anatoa leseni  anasikia, hakuna mahali ambapo pana kidhi kuweka mashine ya kuchezesha michezo ya kubahatisha, wote watoke waende Mijini ambapo kunastahili" alisema Kitundu.

Amesema mchezo huo unasababisha wanafunzi kuwa watoro na wengine kutoroka muda wa masomo.

Amesema licha ya serikali kutoa leseni katika michezo hiyo lakini wananchi hawaitaki kabisa michezo hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Babati Hamisi Malinga amemueleza mkuu wa wilaya kuwa atasimamia agizo hilo lifanyiwe kazi katika maeneo yote ya vijijini ikiwa ni pamoja na kusitisha leseni zilizotolewa kwa ajili ya mchezo huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com