DC IRINGA: "WANAFUNZI WA KIKE MSIJIRAHISISHE TUPUNGUZE UKATILI"


Na Mwandishi Wetu Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela amewataka wanafunzi wa kike kutojirahisisha mpaka kupelekea kufanyiwa vitendo vya ukatili dhidi yao.


Ameyasema hayo leo mkoani Iringa wakati akiupokea Msafara wa kijinsia wa kutokomeza ukatili wa kijinsia uliposimama mkoani hapo.

Ameongeza kuwa vitendo vya kikatili vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku hasa katika familia na vimekuwa vikifumbiwa macho na kumalizana kimya kimya.

"Msijirahisishe watoto wangu mnatupa tabu sana maana tumekuwa tunapambana na vitendo vya ukatili ninyi mnajirahisisha" alisema

Mhe. Kasesela amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la mimba na ndoa za utotoni na ulawiti kwa watoto wa kiume watoto wamekuwa wameharibiwa na kusbabishiwa maumivu na ukatili wa kisaikolojia.

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga katika kuhakikisha inasimamia ustawi wa jamii ikiwemo kuwalinda na vitendo vya kikatili dhidi yao hasa kwa makundi maalum ya wanawake, Watoto na walemavu.

"Tusikae kimya tuseme tutoe taarifa kwa vyombo vya kisheria kuhusu vitendo vya kikatili vinavyotokea katika familia na jamii zetu"alisema.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi Imelda Kamugisha amesema vitemdonvyabukatili.vimekuwa vikitokea kwenye jamii zeru na kwa mujibu wa takwimu wanawake asilimia 30 walio kwenye ndoa wanafanyiwa ukatili wa kijinsia.

"Kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili Serikali imeongeza vituo vya huduma jumuishi na namba ya kutoa ripoti ya vitendo vya ukatili kwa watoto ili kuweza kuchukua hatua katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili" alisema.

Kwa upande wake Wakili kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na udhamini  RITA Janeth Mandawa ametoa wito kwa wanaume kuandika wosia ili kuondokana na vitendo vya kikatili vinavyowakumba wanawake wajane katika jamii zetu ili kuwezesha kuwapa haki zao stahili.

 "Sisi tunahusika na masuala ya wosia kuandika wosia sio kufa ila inasaidia kutoa maelekezo baada ya mume au mke kufariki ili tuondokane na vitendo vya ukatili"alisema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post