Kombora la Pierre-Emerick Aubameyang na bao kutoka kwa kinda Eddie Nketiah yalitosha kwa Arsenal kunyakuwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Everton.
Mechi hiyo ya Jumapili, Februari 23, iliyosakatwa ugani Emirates iliwashuhudia Arsenal wakitoka nyuma na kulaza miamba wa Merseyside.
Dominic Calvert-Lewin aliiweka Everton kifua mbele, dakika moja tu katika mchezo huo kwa kuvurumisha hadi nyavuni kupitia shuti la Sigurdsson. Hata hivyo, Nketiah, alisawazishia Arsenal dakika ya 27 ambaye alitingisha wavu baada ya kumalizia krosi tamu ya Sala.
Aubameyang alibadilisha matokeo hayo kuwa 2-1 dakika sita baadaye, kwa kumchenga Jordan Pickford.
Lakini zikiwa zimesalia sekunde kuingia muda wa mapumziko, Everton walisawazisha bao hilo kupitia kwa Richarlison ambaye aliwasiliana na Bernd Leno na kuhakikisha awamu ya kwanza inaisha sare.
Awamu ya pili ilimshuhudia Aubameyang akiirejeshea Arsenal uongozi kupitia pasi ya Nicolas Pepe kupitia kichwa kutoka upande wa kulia.
Upande zote mbili zilishindwa kuonja wavu kwa mara nyingine tena huku wenyeji wakiondoka na ushindi wa 3-2.