Mnyama aina ya Mamba akiwa pembezoni mwa Mto Wami unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan akiota jua
Wanyama aina ya Twiga wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan kama walivyokutwa
Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakila majani
Sehemu ya watalii wakiwa kwenye gari la wazi wakifanya utalii ndani ya hifadhi hiyo kama walivyokutwa
Mnyama aina ya Ngiri akila majani pembezoni mwa Bahari kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani
Mnyama aina ya Kiboko akiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama walivyokutwa
Makundi ya ndege wakiwa wamejenga viota vyao ndani ya Mto Wami kwenye miti ili kujiepusha na maadui zao kama wanavyoonekana
IDADI
ya Watalii wanaokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan imeelezwa imekuwa
ikiongezeka kutoka 3750 mwaka 2005 hadi kufikia 22890 mwaka 2018.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae wakati
akielezea mafanikio ya Hifadhi hiyo tokea ilipoanzishwa kwake huku akieleza
idadi hiyo imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka.
Alisema
hicho ni kiwango kikubwa kilichoifanya hifadhi hiyo iendelee kukua kutokana na
uwepo wa vivutio vyingi vya utalii ikiwemo upekee wa hifadhi na zilivyo
nyengine hapa nchini.
Akizungumzia
mafanikio ya kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli tokea mwaka 2015 alisema
idadi ya wageni imepanda kutoka 15000 na kufikia idadi ya wageni 22920 ambapo
ni ongezeko la wageni 7900.
Afisa
Utalii huyo alisema kwamba ongezeko hilo limetokana na juhudi kubwa zinazofanywa
na Serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza kwenye ununuzi wa ndege jambo ambalo
linakuza utalii.
Alieleza
kwamba uwekezaji huo wa ndege umesaidia kwa asilimia kubwa watalii kutoka
kwenye nchi zao na kutua moja kwa moja nchini na hivyo kutokutumia muda mwingi.
Akielezea
shughuli za utalii zinazofanyika kwenye hifadhi hiyo alisema kwamba ni utalii
wa kutembea na magari hifadhini,utalii wa matembezo ambapo mtalii anakuwa na
askari kwa ajili ya usalama ambapo unatoa fursa wageni kuona wanyama kwa
ukaribu sana.
Aliongeza
aina nyengine ya utalii ni utalii wa usiku ambapo wanyama awengine jamii ya
Paka huwezi kuwaona mchana maana wanakuwa wamepumzika wakiwemo Simba, Chui,
Fisi ambao usiku mara nyingi wanaweza kuonekana.
Hata
hivyo alisema kwamba kwenye hifadhi hiyo wana wanyama wakubwa wanne ambao
huitwa Big 4 ambao ni Nyati, Tembo, Simba, Chui na mnyama ambaye anakosekana ni
Faru.
“Lakini
hivi sasa niwaambie kwamba wageni wanaoongoza kutembelea hifadhi yetu ni kutoka
nje ya nchi za Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani,wa Rusia na baadhi ya
nchi za ulaya huku akieleza masoko mapya ambayo yameibuka sasa ni Israel,Wahindi
,Wachina”Alisema
Social Plugin