Msemaji wa Familia ya Marehemu Idd Simba, Ahmed Simba, amesema kuwa mwili wa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, utapumzishwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni, lengo likiwa ni kumpumzisha mahali ambapo Baba zake wote walizikwa.
"Sasa hivi tuko hapa Msasani nyumbani kwake, tutaondoka na mwili mpaka Msikiti wa Manyema utaswaliwa pale kisha tutaelekea Magomeni na atazikwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu, anazikwa kule kwa sababu Baba zake wote wamezikwa hapo" amesema Ahmad.
Waziri huyo wa zamani wa Viwanda na Biashara Iddi Simba, alifariki Dunia siku ya jana Februari 13, 2020, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa akipatiwa matibabu
Social Plugin