Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) ambaye pia ni mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro, amefungua mkutano wa siku mbili wa nchi wanachama wa shirikisho hilo unaofanyika jijini Dar es salaam.
IGP Sirro amesema kuwa wakati wa mkutano wao washiriki kutoka nchi 14 Wanachama wa EAPCCO, watajadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaalamu wa namna ya kupambana na ugaidi na uhalifu unaovuka mipaka na kuongeza kuwa suala la mipaka lisiwe kikwazo kwa nchi Wanachama katika kushughulikia makosa mbalimbali.
Social Plugin