Kamati ya haki za kibinadamu ya bunge la Iraq imetoa taarifa ikisema, maandamano yaliyotokea katika sehemu mbalimbali za Iraq katika miezi minne iliyopita, yamesababisha vifo vya watu 536 na wengine elfu 23 kujeruhiwa.
Taarifa hiyo imesema kuanzia Oktoba mosi mwaka jana hadi Januari 30 mwaka huu, maandamano hayo yamesababisha vifo vya waandamanaji 519 na wengine elfu 20 hivi kujeruhiwa, huku askari 17 wakifariki na wengine elfu 3.5 wakijeruhiwa kwa upande wa kikosi cha usalama.
Social Plugin