Na Magreth Kinabo- Mahakama
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema ipo haja ya kutoa taarifa fupi kuhusu kesi zenye mvuto katika jamii ili ziweze kueleweka kwa umma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Majaji wa Mahakama ya Tanzania na Majaji wa Mahakama ya Uingereza lililoanza Februari 3 na linatarajia kumalizika Februari 4, mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K . uliopo jijini Dar es Salaam, Jaji Mkuu alisema majaji ya Uingereza wao tayari wanafanya hivyo.
‘‘Itabidi tubadilike sisi Majaji huenda pale tunadhani kesi zenye mvuto katika jamii, tuanze na sisi kutoa taarifa fupi , ikiwemo kuandika hukumu ili ujumbe uweze kufika kwa wananchi, alisema Jaji Mkuu.
Alisema kesi hizo zinapaswa kutolewa kwa taarifa hiyo zikiwa katika nakala ngumu na laini sambamba na lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Aidha Jaji Mkuu akizungumzia kuhusu kongamano hilo, alisema lina lengo la kushifrikiana na kubadilishana uzoefu kwa kuwa taratibu mbalimbali za kimahakama baina nchi hizo mbili zinafanana.
Aliongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, tayari Majaji 21 na Mahakimu 24 wamepatiwa mafunzo.
Hivyo kupitia ushirikiano huo, utasaidia kuleta matokeo chanya katika maboresho yanayoendelea kwenye Mahakama ya Tanzania na ukiwemo Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania, kuanzia mwaka 2015/16 hadi 2019/20.
Kwa upande wake, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi alisema Mahakama inafanya kazi na nchi zote zilizopo katika Jumuia ya Madola ili kuweza kuboresha utendaji kazi na kuweza kuwa na mifumo bora na kiwango kinachokubalika..
Hivyo kongamano hilo ni fursa litasaidia kuongeza ujuzi kwa Majaji wa Tanzania kuweza kutoa maamuzi hasa katika kesi kubwa za wawekezaji kutoka nje ya nchi..
Dkt. alisema nchi inaongezeka kuwa na wawekezaji wengi wa kigeni , hata katika mahakama zetu kuna mashauri yanayofunguliwa na kampuni za kigeni.
Social Plugin