Picha : JAMBO YATOA MSAADA WA VINYWAJI KWA JESHI LA AKIBA SHINYANGA


Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ ya mkoani Shinyanga imetoa msaada wa katoni 50 za vinywaji kwa wanafunzi wa Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga waliopo katika mafunzo yao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo Ijumaa Februari 21,2020, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Esme Salum amesema kampuni hiyo imeungana na wanafunzi wa Jeshi la akiba kwa kuchangia katika kufanikisha mahafali ya mafunzo yatakayofanyika Machi 4,2020.

“Jambo tumefurahi kuungana na wanafunzi wa jeshi la akiba kwa kuchangia katika kufanikisha mahafali yao ikiwa ni sehemu ya utamaduni wetu tuliojewekea kushirikiana na jamii inayotuzunguka. Tumetoa katoni 50 za vinywaji baridi kati ya katoni hizo 20 ni za maji na 30 ni za juisi mchanganyiko”,amesema Salum.

Akipokea katoni hizo za vinywaji baridi, Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala ameishukuru Kampuni ya Jambo kwa kuwaunga mkono kufanikisha sherehe ya jeshi la akiba.

“Tuliwaandikia barua Jambo ya kuomba msaada watuchangie katika mahafali yetu ya jeshi la akiba.Kwa kweli tunawashukuru sana Jambo wamejitoa kwa moyo mmoja,wametupatia maji katoni 20 pamoja na juisi katoni 30.

Tunawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika sherehe yetu ya jeshi la akiba Mungu awabariki sana,kazi yenu iendelee kubarikiwa”,amesema Kamala.

Jumla ya wanafunzi 143 wa Jeshi la akiba kutoka wilaya ya Shinyanga walioanza mafunzo yao Novemba 4,2019 wanatarajia kumaliza mafunzo yao Machi 4,2020.
Kushoto ni Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akishikana mkono na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala wakati akimkabidhi katoni 50 za vinywaji baridi kuchangia mahafali ya wanafunzi wa Jeshi la Akiba yatakayofanyika Machi 4,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akishikana mkono na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala wakati akimkabidhi katoni 50 za vinywaji baridi kuchangia mahafali ya wanafunzi wa Jeshi la Akiba.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum (wa pili kushoto) akikabidhi vinywaji baridi kwa viongozi wa kamati ya sherehe mahafali ya Jeshi la akiba wilaya ya Shinyanga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe Sarah Stephen,wa kwanza kulia ni Katibu wa sherehe Aderick Godfrey akifuatiwa na Mhasibu wa sherehe Martha Charles.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akimwelezea Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na baadhi ya wanafunzi wa Jeshi la Akiba namna kiwanda cha Jambo kinavyoendesha shughuli za uzalishaji wa vinywaji baridi.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akieelezea namna wanavyozalisha vinywaji baridi.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akionesha muonekano wa chupa ya kuwekea vinywaji kabla ya kuingizwa kwenye mitambo.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na baadhi ya wanafunzi wa Jeshi la Akiba  wakiangalia namna uzalishaji wa vinywaji baridi unavyofanyika.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akiendelea kuwatembeza kiwandani wageni wake.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akiendelea kueleza namna kiwanda cha Jambo kinavyoendesha shughuli za uzalishaji wa vinywaji baridi.
Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum akiteta jambo na Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala baada ya kutembelea kiwanda cha Jambo.

Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum.  akimkaribisha ofisini kwake Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala (kulia).
 Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum. (wa pili kulia) akielezea namna Kampuni yao inavyoshirikiana na jamii kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Prouducts kwa kuchangia katoni 50 za vinywaji baridi ili kufanikisha mahafali ya Jeshi la Akiba.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala  akiagana na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum.
Msaidizi Ofisi ya Jeshi la Akiba wilaya ya Shinyanga,Sajenti Geofrey Kamala na wanafunzi wa Jeshi la Akiba wakipiga picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ Esme Salum.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post