Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuita kwa mahojiano mwanaharakati huru Cyprian Musiba baada ya kutoa tuhuma mbalimbali za kutishiwa kuuawa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 24,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Musiba kupitia baadhi ya magazeti hapa nchini amechapisha taarifa za kulalamika kutishiwa kuuawa na baadhi ya wanasiasa .
Hivyo Kamanda Muroto ametoa Rai kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa habari za makosa ya jinai kwenye vyombo vya habari bila kujulisha vyombo vya dola na jeshi hilo limemuita Musiba kwa Mahojiano zaidi dhidi ya Malalamiko yake.
Social Plugin