Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: LA PRINCE CHARITY MOVEMENT, FRIENDS OF DR TULIA,WADAU WASHEREHEKEA VALENTINE'S DAY KWA KUMWAGA MISAADA HOSPITALI ,KAMBI YA WAZEE KOLANDOTO



Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
La Prince Charity Movement, Friends of Dr Tulia kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Shinyanga mjini, wametoa misaada mbalimbali kwenye kambi ya kulea wazee Kolandoto, pamoja na hospitali ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapenda nao 'Valentine's day' kwa kutoa misaada kwa wahitaji.


Zoezi hilo limefanyika leo Ijumaa Februari 14, 2020 siku ya wapendanao duniani, kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji wakiwemo wazee wanaolelewa kwenye kambi ya wazee Kolandoto na hospitali ya eneo hilo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akimwakilisha mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko.

Akizungumza kwenye zoezi hilo Mkurugenzi wa La Prince Athanas William, amesema wameamua kusherehekea siku ya wapendanao 'Valentine's day' kwa kufanya jambo pamoja na Taasisi ya Friends of Dr Tulia, wafanye kitu gani, na kuamua kushirikisha wadau wengine wa maendeleo ili kwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee na wagonjwa katika hospitali ya Kolandoto kwa kuonyesha upendo.

“Sisi kama La Prince Charity Movement pamoja na taasisi ya Friends of Dr Tulia kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, tulikaa na kujadili tufanye jambo la kusaidia watu wenye uhitaji kwenye siku hii ya wapenda nao, ili kuonyesha upendo kwao na kujiona jamii ipo pamoja nao,”alisema William.

“Napenda kutaja wadau wengine ambao tumeshirikiana nao, Thubutu Afrika, TVMC,Benki ya CRDB, Ommy Fashion, Lulekia, Jambo Food Products Co, Dellah Car Traders, Gven Wear, Big Five, Sigla, Tausi Cofee, Little Treasures, Skauti, SSG Security, Ofisi ya Fatihu Advocate, Tawlae, Save The Children,Malunde 1 blog pamoja na Umoja wa Vijana CCM UVCCM na wadau wengine”,ameongeza.

Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Friends of Dr Tulia mkoani Shinyanga Shabani Wisandara, ametaja misaada mbalimbali ambayo wameitoa kwenye kambi hiyo ya wazee Kolandoto, zikiwamo nguo, viatu, vyakula, mafuta, juice, sabuni za kufulia, pamoja na wagonjwa kuwapatia juice, maji ya kunywa na sabuni.

Aidha amesema mbali na kutoa msaada huo wa chakula na mavazi, pia wameweza kuchangisha fedha kiasi cha Shilingi 240,000, kwa ajili ya kuwakatia kadi ya bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa wazee wote 17 ambao wanaishi kwenye kambi hiyo ya Kolandoto, huku akiahidi mwaka 2021 atawakatia tima bima hiyo kwa fedha yake.

Kwa upande wake mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akimwakilisha mkuu wa wilaya Jasinta Mboneko, amewapongeza wadau hao wa maendeleo kwa kubuni kitu cha msingi sana, ambapo wangeweza kusheherekea siku ya wapenda nao kwa kufanya starehe, lakini wakaamua kusaidia watu wenye uhitaji, jambo ambalo linahitaji kuingwa ikiwa watu wanaohitaji misaada wapo wengi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkurugenzi wa La Prince Athanas William akizungumza kwenye kambi ya wazee Kolandoto leo Februari 14,2020 wakati wadau wa maendeleo walipotembelea kambi hiyo kwa ajili ya kutoa misaada/zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao 'Valentine's day'. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa taasisi ya Friends Of Dr Tulia Shabani Wisandara akizungumza kwenye kambi ya wazee Kolandoto leo Februari 14,2020 wakati wadau wa maendeleo walipotembelea kambi hiyo kwa ajili ya kutoa misaada/zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao 'Valentine's day'.
Msanii wa kizazi kipya Belle 9 akizungumza kwenye kambi ya wazee Kolandoto manispaa ya Shinyanga leo Februari 14,2020 wakati wadau wa maendeleo walipotembelea kambi hiyo kwa ajili ya kutoa misaada/zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao 'Valentine's day'.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza kwenye kambi ya wazee Kolandoto leo Februari 14,2020 wakati wadau wa maendeleo walipotembelea kambi hiyo kwa ajili ya kutoa misaada/zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao 'Valentine's day'.
Afisa ustawi mkazi kambi ya wazee Kolandoto Sophia Kang'ombe akitoa taarifa fupi juu ya kambi  ya wazee Kolandoto leo Februari 14,2020 wakati wadau wa maendeleo walipotembelea kambi hiyo kwa ajili ya kutoa misaada/zawadi kwa wazee hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wapendanao 'Valentine's day'.
Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akipongeza wadau hao kwa msaada walioutoa kwa wazee kwenye kambi hiyo ya Kolandoto.
Wadau wakishusha misaada kwenye kambi ya wazee Kolandoto.
Baadhi ya misaada ambayo wamepewa wazee kwenye kambi hiyo ya Kolandoto.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na misaada mbalimbali kwa ajili ya wazee wa kambi ya wazee Kolandoto


Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na misaada mbalimbali kwa ajili ya wazee wa kambi ya wazee Kolandoto
Mwenyekiti kambi ya wazee Kolandoto Samola Maganga akitoa shukrani kwa niaba ya wezanke juu ya msaada waliopewa.
Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Kolandoto wakiwa kwenye zoezi la kupewa misaada mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Kolandoto wakiwa kwenye zoezi la kupewa misaada mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Wadau wa maendeleo wakielekea kutoa zawadi ya vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika hospitali ya Kolandoto.
Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye hospitali ya Kolandoto tayari kwa kutoa zawadi kama ishara ya upendo kwao.
Msanii wa kizazi kipya Belle 9 akitoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali ya Kolandoto.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Ngangala akitoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali ya Kolandoto.

Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge na Meneja Masoko wa Kampuni ya Dellah Car Traders Athuman Mbelwa wakitoa zawadi kwa mgonjwa katika hospitali ya Kolandoto.

Msanii wa kizazi kipya Belle 9 awali akiongoza zoezi upandaji miti katika kambi ya wazee ya Kolandoto.
Wadau wa maendeleo wakiendelea kupanda miti katika kambi ya wazee Kolandoto.
Wadau wa maendeleo wakiendelea kupanda miti katika kambi ya wazee Kolandoto.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
oezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Mkurugenzi wa La Prince Athanasi William akitoa Cheti cha Pongezi kwa Kampuni ya Jambo kwa kushiriki kuchangia kutoa msaada kwenye Kambi ya wazee Kolandoto.
Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akitoa vyeti vya Pongezi kwa wadau walioshiriki kufanikisha zoezi hilo la utoaji misaada kwenye kambi ya wazee na wagonjwa katika hospitali ya Kolandoto.
Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala akimkabidhi cheti cha pongezi Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale.
Ommy Fashion akikabidhiwa cheti cha pongezi.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia,Ansila Benedict akipokea cheti cha pongezi
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji wa vyeti likiendelea.
Mkurugenzi wa Ney Fashion,Neema Chacha akipokea cheti
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear akipokea cheti
Mgeni Rasmi Afisa tawala wa wilaya ya Shinyanga Beda Kamala, akitoa cheti cha Pongezi kwa Mwandishi wa habari wa Malunde 1 blog Salvatory Ntandu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Malunde Media inayomiliki Mtandao wa Malunde 1 Blog 
Wadau wa maendeleo wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutoa zawadi kwenye kambi ya wazee Kolandoto.

Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com