Baraza la madiwani la halmashauri ya ushetu wilayani kahama mkoani shinyanga limeshauri kufanyika kwa matengenezo ya haraka ya mitambo ya ujenzi wa barabara ya halmashauri hiyo ambayo imeharibika ili kufanya ukarabati wa miundo mbinu ya barabara ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Baraza hilo limetoa ushauri huo febuari 6 mwaka huu katika, kikao cha robo ya pili ya mwaka wa fedha kilichofanyika katika makao makuu ya halmashauri hiyo Nyamilangano na kuhudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo na wananchi mbalimbali.
Hoja hiyo imetolewa na Kurwa Shoto diwani wa kata ya Bukomela ambapo alisema kuwa halmashauri hiyo inapaswa kufanya matengenezo haraka ya mitambo yake ili kutatua changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya barabara.
“Tusikimbilie kukodisha mitambo yetu bali tuifanyie matengenezo kwanza ile iliyoharibika kabla hatujapanga kuikodisha haiwezekani tukawa na mitambo isiyokuwa inafanya kazi kisa ni mibovu”alisema Shoto.
Kwa upande wake diwani wa kata ya mapamba, Yohana Mango alishauri halmashauri iongeza nguvu katika maeneo yenye changamoto ya barabara ambazo hazipitiki kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.
“Tumekaribia kuanza msimu wa mavuno kwa mazao kama mahindi,kataranga na Tumbaku hivyo ni budi tukahakikisha halmashauri yenu inakuwa na barabara zenye kiwango na kupitika na kuongeza mapato ya ndani kutoka na ushuru unaotarajiwa kukusanywa”alisema Mango.
Awali akitoa taarifa ya utengenezaji wa Mitambo hiyo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Matomora alisema mitambo hiyo imeshatengenzwa na kwa sasa imebaki kwenye maeneo ambayo wanatengeneza barabara na sio kwamba imeharibika kama inavyodhaniwa.
“Ushetu tunajivunia kuwa na mitambo ya ujenzi wa barabara kwani mpaka sasa tumeweza kutengeneza barabara kilomita 1030 za changarawe ikilinganishwa na halmashauri zingine katika mkoa wa Shinyanga alisema Matomora.
Nae Katibu Tawala msaidizi wa serikali za mitaa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Alphose Kasanyi aliwataka madiwani hao kujivunia kuwa na mitambo yao ya kutengenezea barabara na wanapaswa kuitunza ili iweze kuleta tija.
“Mkoa wa Shinyanga nyinyi ndio halmashauri pekee yenye kujitosheleza kwa kuwa na mitambo ya kutengenezea barabara hebu jikiteni kufunga njia ambazo hazipitiki ili kuwawezesha wananchi mnao wahudumuia kupata huduma mbalimbali kwa wakati” alisema Kasanyi.
Katika kikao hicho cha kawaida cha baraza la madiwani robo ya pili ya mwaka wa fedha 2019/20 Madiwani wa kata 20 katika halmashauri hiyo wamewasilisha taarifa za maendeleo za kata zao ili ziwezekufanyiwa kazi na wataalamu wa halmashauri ya Ushetu.
Mwisho.
Social Plugin