MAHAKAMA KENYA YAZUIA WANANCHI KUSAJILIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE


Mahakama Kuu Kenya imesitisha kutekelezwa kwa mfumo wa usajili wa wananchi kwa njia ya alama za vidole hadi hapo sheria ya kulinda taarifa itakapopitishwa.

Mbali na kuzuia utekelezaji huo, mahakama imesema kuwa kukusanya taarifa za eneo (GPS) na vinasaba (DNA) ni kinyume na katiba ya nchi.

Serikali ya Kenya imekuwa ikikusanya taarifa mbalimbali katika usajili huo ikiwa ni pamoja na alama za vidole, taarifa za familia, na eneo kamili mtu analoishi.

Wakati wa zoezi hilo ambalo serikali ilisema ni la lazima wale wote ambao hawatojiandikisha hawatopata huduma za msingi za serikali kama vile pasi ya kusafiria (passport), na cheti cha kuzaliwa.

Mahakama imezuia zoezi hilo kwa kile ilichoeleza kwamba wananchi wanaweza kujikuta katika hatari isiyorekebishika endapo taarifa zilizokusanywa zitatumiwa vibaya.

Majaji watatu wa mahakama hiyo waliamuru kusitishwa kwa mpango huo unaofahamika kama Huduma Namba hadi sheria ya kina ya kulinda taarifa zinazotolewa na wananchi upitishwe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post