MAHAKAMA YAFUTILIA MBALI UCHAGUZI WA RAIS WA MALAWI ULIOMPA USHINDI PETER MUTHARIKA

Mahakama ya kikatiba ya Malawi imefuta matokeo ya uchaguzi uliomuweka madarakani, Peter Mutharika.


Imesema uchaguzi huo  uliofanyika Mei 21, 2019 haukuwa huru na haki, hivyo imeamuru  urudiwe ndani ya siku 151, mshindi lazima apate kura zaidi ya nusu ya idadi ya waliopiga kura.

Majaji waliotoa uamuzi huo wakiongozwa na Healey Potani wameeleza kubaini  Tume ya Uchaguzi Malawi (MEC) kupokea ripoti 147 zinazoonyesha kuwa matokeo hayo hayakuwa sahihi kutokana na kasoro mbalimbali, ikiwa ni pamoja na baadhi ya matokeo kubadilishwa.

Mutharika alishinda kwa asilimia 38 ya kura zote akifuatiwa na Lazarus Chakware asilimia 35 na Saulos Chilima aliyewahi kuwa makamu wa rais ambaye alipata asilimia 20.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post