Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KAMATI YA SIASA CCM MKOA WA SHINYANGA YATEMBELEA MRADI WA MAJI WA MWAWAZA - NEGEZI...YAIPONGEZA SHUWASA KASI YA UJENZI


Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa imetembelea Mradi wa Mwawaza - Negezi katika Manispaa ya Shinyanga na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Mradi huo wa Maji ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.

Akizungumza leo Februari 11,2020 katika eneo la ujenzi wa Tenki la Maji katika kata ya Mwawaza,Mwenyekiti CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa ameeleza kufurahishwa na kasi ya ujenzi mradi huo wa maji.

“Niwapongeze SHUWASA kwani naona ujenzi huu wa mradi unaendelea vizuri. Naipongeza serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM,kwani wakati wa kampeni za uchaguzi tuliahidi kuwaletea maji safi na salama wananchi”,alisema Mabala.

“Ujenzi wa mradi wa maji kata ya Mwawaza ni sehemu ya ahadi tulizoahidi.Ni matumaini yangu kuwa pindi mradi huu utakapokamilika wananchi wa Mwawaza na vijiji jirani watanufaika na mradi huu wa maji”,alisema Mabala.

Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi, Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA, alisema SHUWASA inasimamia na kujenga mradi huo wa maji kwa kutumia wataalamu wa ndani “Force account” ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.

Alisema mradi wa maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020 ukitarajia kunufaisha wananchi wa kijiji cha Mwawaza,Negezi na Bugimbagu na vijiji jirani.

“Mradi huu unahusisha ujenzi wa tenki na mtandao wa maji safi.SHUWASA inaendelea na utekelezaji wa mradi huu ambapo kwa sasa ujenzi wa tenki kwa mradi wa Mwawaza – Negezi umefikia hatua ya ukuta kwa tenki lenye ujazo wa lita 200,000 na hatua ya ufungaji wa nondo za ukuta kwa tenki dogo lenye ujazo wa lita 50,000”,alisema Mhandisi Katopola.

Alisema ujenzi wa matenki unaosimamiwa na SHUWASA kwa kushirikiana na RUWASA unatarajia kugharimu fedha za Kitanzania shilingi Milioni 130 hadi kukamilika kwake.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA akimwelezea Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa (wa kwanza kulia) kuhusu ujenzi wa mradi wa Maji Mwawaza - Negezi wakati Kamati ya Siasa CCM mkoa wa Shinyanga ilipotembelea mradi huo wa maji leo Jumanne Februari 11,2020 ikiwa ni sehemu ya ziara yao kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akiipongeza SHUWASA kwa kasi yao katika ujenzi tenki ikiwa ni sehemu ya utekelezaji ujenzi wa mradi wa Mwawaza - Negezi. Wa Pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Mhe. Nyabaganga Talaba.
Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA akiieleza Kamati ya Siasa CCM mkoa wa Shinyanga kuhusu mradi wa maji wa Mwawaza - Negezi.
Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola akionesha tenki lenye ujazo wa lita 200,000 ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia hatua ya ukuta.
Wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Shinyanga na viongozi mbali wa serikali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa katika eneo panapojengwa tenki la maji kwa ajili ya mradi wa maji wa Mwawaza - Negezi.
Muonekano hatua ya ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Mwawaza  Negezi ulipofikia.
Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola akimuongoza Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa (nyuma) kupanda juu ya tenki la Maji linalojengwa katika kata ya Mwawaza kwa ajili ya mradi wa Maji wa Mwawaza - Negezi.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa (nyuma) kupanda juu ya tenki la Maji linalojengwa katika kata ya Mwawaza kwa ajili ya mradi wa Maji wa Mwawaza - Negezi. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Shinyanga,Richard Msanii akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya na Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Mhe. Abubakar Gulam akijiandaa kupanda juu ya tenki hilo.Wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akifuatiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Geofrey Mwangulumbi na wajumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola akimunesha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa hatua iliyofikiwa ujenzi wa tenki la Maji linalojengwa katika kata ya Mwawaza kwa ajili ya mradi wa Maji wa Mwawaza - Negezi.
Muonekano wa tenki hilo,hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza juu ya tenki la maji mradi wa Maji Mwawaza - Negezi na kuwahamasisha viongozi wa SHUWASA kusimamia kikamilifu mradi huo ukamilike kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma ya maji safi na salama.
Wajumbe wa kamati ya siasa CCM mkoa wa Shinyanga wakiwa juu ya tenki la maji.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akishuka kwenye tenki la maji linaloendelea kujengwa katika kata ya Mwawaza ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa maji wa Mwawaza- Negezi unaosimamiwa na SHUWASA kwa kushirikiana na RUWASA.
Mafundi wakiwa juu ya tenki hilo linaloendelea kujengwa.
Wafanyakazi wa SHUWASA na diwani wa kata ya Mwawaza,Mhe, Juma Nkwabi (wa tatu kulia) wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye tenki hilo la maji linaloendelea kujengwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com