Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegoma kuzungumzia kuzuiwa kuingia nchini Marekani kwa maelezo kuwa kuna siku atalizungumzia suala hilo.
Makonda ametoa majibu hayo leo Ijumaa Februari 14, 2020 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds
Katika kipindi hicho ambacho Makonda alikuwa anazungumzia mambo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam, aliulizwa kama tayari ameshapokea barua kutoka Marekani ya kumpiga marufuku kuingia nchini humo.
Akijibu sali hilo, Makonda amesema kuwa leo alifika katika kipindi hicho kuzungumzia masuala ya kiserikali si binafsi.
“Hapa nimekuja kama mkuu wa mkoa, subiri nikija binafsi tutajadiliana, nimekuja kama Serikali,” amesema
Tarehe 1, February 2020 Marekani ilieleza kumzuia Makonda kuingia Marekani pamoja na mkewe, Mary na kwamba sababu ni tuhuma za kushiriki kukandamiza haki za binadamu.
Social Plugin