MAMA SALMA KIKWETE ALIA NA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MKOANI LINDI

     Wakati taharuki ya mafuriko mkoani Lindi ikiendelea mbunge wa kuteuliwa na Rais Mama Salma kikwete na mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne amefika mkoani Lindi na kuongozana na viongozi wa chama cha mapinduzi kwenda kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko.

      Katika ziara hiyo Mama Salma kikwete amefika katika kambi ya Nanjime na mji mwema yenye jumla ya wahanga 482 na kuwafariji wahanga hao.

  "Kwa niaba ya wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha mapinduzi walinipatia  salamu za pole ili nizifikishe kwenu, tunaungana kuwapa pole na kuwahakikishia kuwa tuko pamoja nanyi kwa hali na mali katika wakati huu mgumu mnaoupitia"

   "Niwaombe saana wadau mbalimbali,viongozi, wafanyabiashara na yeyote aliyeguswa kujitoa kwa moyo kuwasaidia ndugu zetu hawa walio kwenye hali mbaya hivi sasa"

Sambamba na salamu hizo za pole, Mama Salma kikwete amekabidhi vifaa vya kuwasaidia wahanga wa mafuriko Bati 500, Doti za kanga 100,Matrubai,viatu pea 50, sabuni Miche 50,Miswaki na dawa za Meno,Nguo za kiume na chakula katika ofisi ya mkuu wa wilaya.

     Akiongea katika kambi hiyo mganga Mfawidhi wa kituo cha kitomanga Dr. Gidion Kategugwa ameishukuru serikali ya mkoa kwa jitihada wazozionyesha kwa kuleta madawa kwa wakati yanayowarahisishia kutibu wagonjwa huku akisema changamoto walionayo ni magonjwa ya matumbo na malaria kwani changamoto ya neti ni kubwa hivyo ameiomba serikali na wadau mbalimbali kufanya jitihada za haraka za upatikanaji wa neti kwa wahanga.

  Kwa upande wa wawakilishi wa wahanga Bwana Bakari Issa Mkulang'ombe Mkazi wa Kijiji cha mkwajuni kitongoji cha Nanjime Ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwaokoa na kuiomba serikali kuwasaidia kwa haraka huduma ya chakula,matrubai,mavazi na chakula huku akiomba serikali kuwapatia mbegu za mazao ya muda mfupi ili waweze kujikwamu kwa baadae.

  Nae Fatuma Ismail Nantima amewaomba wadau kuwasaidia mavazi kwa wakina mama na sare za shule kwa watoto ili waweze  kuendelea na masomo wakati jitihada zingine zinaendelea.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post