Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMLAKA YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI [TIRA ] YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI UMUHIMU WA BIMA KATIKA JAMII



Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa bima nchini [TIRA]imetoa Mafunzoya kuwajengea uwezo Wanahabari umuhimu wa bima katika jamii  kwani ni moja ya suluhisho kwa Majanga.



Akiwasilisha mada mbalimbali katika Mafunzo hayo jijini Dodoma,Mkurugenzi wa kuendeleza soko la bima na utafiti ,mamlaka ya Usimamizi wa bima Tanzania,Bi,Adelande  Muganyizi amesema bima husaidia kupunguza maumivu ya majanga mbalimbali ikiwa  ni pamoja na majanga ya moto,ajali,ukame,na mafuriko hivyo wanahabari wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri  katika kuelimisha jamii umuhimu wa bima kwani huondoa umasikini.



“Majanga hayabigi hodi lakini bima inasaidia kupunguza sana maumivu yaliyotokana na majanga ,hivyo  tunatakiwa tuelewe sana haki ya usalama katika mali zetu pindi tunapokumbwa na majanga kwa hiyo tunapoongelea suala la bima ni usalama wa afya,Usalama wa mali zetu”amesema.



Aidha,Bi.Muganyizi ameanisha kanuni za msingi za  mkataba wa bima ni pamoja na kuwepo na uhusiano unaotambulika kisheria[Insurable interest],uaminifu wa hali ya juu[ultmost  faith], kumrejeshea mkata bima thamani halisi kabla ya janga kutokea pamoja na kuchangia hasara endapo mali moja imechangiwa na makampuni ya bima zaidi ya moja.



Akizungumzia kuhusu bima ya lazima,Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa bima[TIRA]kanda ya kati Stella Rutaguza amesema kwenye magari ya usafiri wa umma kila abiria aliyebebwa anatakiwa awe amekatiwa bima.



“Tukija kwenye suala hili naona kama kuna changamoto kidogo ,lakini kuhusu bima ya lazima inatakiwa kila abiria aliyebebwa kwenye gari la usafiri wa umma awe amekatiwa bima na mwenye jukumu hilo ni mmiliki wa gari husika,kama gari lako lina uwezo wa kibeba abiria 55 na sheria inataka hivyo hivyo ukate bima ya watu wa idadi kama hiyo”amesema .
Pia,Rutaguza amesema moja ya kanuni kubwa  ya bima ni kuwa hairuhusiwi kuikatia bima mali isiyokuwa ya kwako hata kama ni ya ndugu  huku akitaja aina mbalimbali za bima zikiwa ni pamoja na bima za kilimo,bima za ndoa,bima za dhima za umma ,bima za makosa ya kitaaluma ,bima za wizi ,bima za waajiriwa  ,bima za maisha,bima za elimu  na bima za vifo.



Meneja usimamizi wa Maendeleo ya Masoko ,Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa bima Tanzania[TIRA]Bw.Edgar Shao amesema TIRA ina jukumu la kusajili kampuni za bima pamoja na kutoa elimu kwa wananchi


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com