MbungewaJimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka aliyenyanyua mikono akitoa ufafanuzi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula (mwenyemiwani) wakati alipotembelea kwenye mradi mkubwa washamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo kulia kwa Mangula ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa (pichana John Mapepele)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula akikagua Mkorosho kwenye mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku saba katika Mkoa wa Singida(Pichana John Mapepele
Makamu Mwenyekitiwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula akikata keki maalum ya miaka
43 ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha
tathmini na majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani Singida kwenye ukumbi wa maktaba wilayani Manyoni leo kulia ni Mwenyekitiwa
CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma kilimba kushoto ni Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Manyoni Jumanne Mahanda anayefuata Katibu wa
CCM Mkoa wa Singida AlexndrinaKatabi(Pichana John Mapepele)
Umati
wa wanachama wa CCM uliohudhuria mkutano
wa Makamu Mwenyekitiwa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula(Picha na John Mapepele)
Apongeza Mkoa wa Singida
Na John Mapepele
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara,
Philipo Japhet Mangula amewataka
watanzania kutochezea amani na
kuyumbishwa na wanasiasia na
badala yake waione amani walio nayo kama
mtaji mkubwa wa kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Mangula ameyasema haya leo katika ukumbi wa maktaba Manyoni
wakati alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba kwenye Mkoa wa Singida
ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa
nchi chache duniani ambayo imebahatika kuwa amani katika kipindi chote kutokana
na kazi nzuri iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema hivyo ni wajibu wa kila mwananchi
mzalendo kuilinda kwa kuwa watu wengi hawapendi kuona Tanzania ina amani na kupiga maendeleo ya haraka kama
inavyofanya sasa.
“Ndugu zangu hata tukichukulia mfano mdogo tu, katika kipindi
cha miaka 75 ambayo tulitawaliwa na Wajerumani na Waingereza kwenye Wilaya yote
ya Manyoni hatukuwa hata na Shule mmoja
ya Sekondari lakini leo tuna zaidi ya
shule 30 katika kipindi kifupi, je hayo siyo maendeleo makubwa ?” alihoji
Mangula
Alisisitiza kuwa mapinduzi
makubwa ya kiuchumi
yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli yanatokana na msingi
imara uliojengwa ambao ni amani na kwamba wachafuzi wa kubwa wa amani dunani kote ni wanasiasa ambao wamekuwa wakisukumwa na tamaa ya
madaraka ambapo yakitokea wanaoumia
ni watoto, wazee na akina mama.
Akitolea mfano wa machafuko ya kisiasa ya Rwanda ya mwaka 1994
alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo, alishuhudia wimbi kubwa la watoto na akina
mama wakiteseka na kufa njiani wakati
wakijaribu kukimbia nchi yao kunuisuru
maisha yao.
“Nilishuhudia mama akina
mama wakitanda kanga na kumsaidia mama
mwenzao kujifungua mtoto pembeni mwa barabara na baada ya kujifungua tu
wakaendelea na safari, kwa kweli huwa sipendi kukumbuka hali ile maana ni
hatari na ukatili usioelezeka” aliongeza Mangula
Akiwa katika mkutano huo
amesisitiza suala la uadilifu na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za
chama cha Mapinduzi ambapo amesema
vitendo vyoyote vya rushwa na wagombea kuanza kujipitisha kabla ya kipindi
rasmi cha kuchukua fomu za kugombea na kuanza mchakato wa uchaguzi hakikubaliki
na kusisitiza kuwa chama kitachukua hatua kwa wote watakao bainika kufanya
hivyo.
Aidha Kamati za Siasa katika maeneo husika zitakazoshindwa
kuwachukulia hatua wanachama watakaofanya makosa zitaadhibiwa.
Akiwa katika ziara hiyo ametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali
ya Mkoa wa Singida ambapo mradi wa mwisho alioutembelea ni mradi mkubwa wa
shamba la pamoja la Korosho lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 12000 eneo la
Masagati kwenye Wilaya ya Manyoni na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali
katika kuleta mapinduzi makubwa ya
kilimo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.
Amesema alama ya Chama Cha Mapinduzi ni jembe na nyundo ambapo
amesema jembe ni alama ya mkulima na
nyundo ni mfanyakazi hivyo CCM inaamini kuwa
wakulima na wafanyakazi
wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi yao na kuwa mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania yameletwa
na kilimo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka
akimwelezea Mangula kwenye shamba la
Korosho la Masagati ameshukuru Serikali ya Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa
Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kushirikisha wananchi katika kuwabadili
mawazo na mtazamo wa kutafuta maendeleo ya kweli kwa kulima shamba la pamoja la korosho ambapo
amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Mhe. Mtuka amesema kutokana na utafiti uliofanyika na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya
Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya
Kilimo Kanda ya Kati uliofanyika kuanzia
mwaka 2002, matokeo ya utafiti huo
yalionyesha kuwa hali ya hewa na udongo
vinafaa kwa kilimo cha korosho hivyo wakaanza kuwahamashisha wananchi kulima
zao hilo
“ Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri tuliamua
kuanzisha zao la korosho kimkakati ili kuchochea kwa kasi kubwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja
wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla’”
aliongeza Mhe. Mtuka
Aidha,alipongeza Serikali
ya Mkoa kwa kubuni wazo la kuanzishwa kituo kwa kikubwa cha hija duniani cha Bikira Maria katika eneo la Sukamahela, sehemu ambayo ni
katikati ya nchi ya Tanzania kwa ajili
ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuhiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles
Fussi amesema kuwa kazi zinazoendelea
katika eneo hilo kwa sasa ni kuhamasisha wakulima wajiunge na kilimo cha korosho, kuendelea
kutoa huduma za ugani kwa wakulima ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya viuatilifu kwa
kushirikiana na TARI na Bodi ya Korosho, kuendelea kazi ya kusafisha na kugawa
mashamba kwa wakulima na kuzalisha miche
bora korosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson
Mwagisa amemhakikishia Mangula kuwa
serikali itaendelea kusimamia
kikamilifu na kuwa hamasisha wananchi
kutoka sehemu mbali mbali nchini kuja
kuwekeza katika kilimo cha korosho kwenye eneo hilo kwa kuwa mradi
huo na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya
ya Manyoni na Taifa kwa ujumla.
Ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na udhibiti wa
visumbufu kama magonjwa na wadudu,udhibiti wa ubora wa korosho kutokana na usimamizi wa
karibu, upatikanaji wa uhakika wa soko katika eneo la mradi,kurahisisha
upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuhudumia eneo kubwa kwa wakati
mmoja na chanzo kikuu cha malighafi za
viwanda vya kusindika korosho.
Manufaa mengine ya mradi ni kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri
kupitia ushuru na kodi za biashara mbalimbali zitokanazo na ongezeko la uchumi
katika sekta mtambuka zinazoendana na zao hilo, hali ya maisha kuboreka ikiwa ni pamoja na ujenzi wa makazi bora na
kuongezeka uhakika wa chakula
katika kaya.