Marekani na kundi la wanamgambo wa Taliban leo wametia saini makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya miaka 18 nchini Afghansitan na kuwezesha Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo.Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Doha, Qatar.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo pamoja na msemaji wa kundi la Taliban mjini Doha, Suhail Shaheen walikuwepo wakati makubaliano hayo yaliposainiwa.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mike Pompeo ametoa wito kwa Taliban kuheshimu ahadi ilizotoa ikiwa ni pamoja na kukomesha mahusiano yake na makundi ya itikadi kali.
Chini ya mkataba huo Marekani itaanza kuondoa wanajeshi wake kwa makubaliano ya Taliban kuzuia mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Afghanistan.