MBUNGE ATAKA WABAKAJI WAHASIWE....SERIKALI YAGOMA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Serikali imesema haiwezi kuongeza adhabu kali kwa wabakaji  zikiwemo adhabu za kuhasiwa  kwani zilizopo ni kali na zinatosha.

Hayo yamesemwa leo Feb.4.2020  jijini Dodoma na Waziri wa katiba na sheria  Balozi.Dkt.Augustne Mahiga wakati akijibu swali la  nyongeza la mbunge wa viti Maalum [CCM]Mhe.Zainab Katimba aliyehoji kutokana na vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike hususan ubakaji kuendelea kuripotiwa mara kwa mara ,je,serikali haioni namna ya kuongeza adhabu kali dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo.

Akijibu  swali hilo,Waziri wa Katiba na Sheria ,Balozi.Dkt.Augustine Mahiga amesema adhabu zilizopo kwa sasa ni kali kwani mtu aliyefanya kosa la ubakaji ni miaka 30 mpaka wengine wanafia magerezani.

Akilitolea ufafanuzi zaidi   juu ya suala hilo,Mwanasheria  mkuu wa Serikali Dkt.Adelardus  Kilangi amesema pendekezo la kuhasiwa litapekekea kuvunja katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika ibara  ya 13,ibara ndogo ya 6 ambapo inaeleza ni marufuku kwa mtu kuteswa,kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu  zinazomtesa au kumdhalilisha .

Naye Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy Mwalimu amesema sheria peke yake hazitoshi na kinachotakiwa ni wazazi na walezi kutimiza wajibu katika ulinzi na malezi kwa watoto.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post