Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Ruth Mollel ameishauri Serikali kuweka nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali kwa sababu wana hali mbaya.
Ruth ametoa kauli hiyo leo Jumanne Februari 4, 2020 wakati akichangia taarifa tatu za utekelezaji wa shughuli za kamati za Utawala na Serikali za Mitaa, Katiba na Sheria pamoja na Sheria Ndogo.
Ruth amesema katika taarifa zote alizosoma hakuna sehemu wamezungumzia kundi kubwa la watumishi wa umma ambalo ni raslimali watu.
Amesema kwa muda wa miaka minne hawajawahi kuongezewa mishahara na kwamba hilo jambo amekuwa akilisema mara nyingi.
Social Plugin