Misri imefanya mazishi ya heshima za kijeshi ya aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak, ambaye aliitawala nchi hiyo kwa miongo mitatu kabla ya kuondolewa katika mwaka wa 2011 kupitia wimbi la vuguvugu la mageuzi katika ulimwengu wa Kiarabu.
Hafla hiyo ya mazishi, ilihusisha kufyatuliwa mizinga na jeneza lake kubebwa kwenye msafara wa farasi kuashiria mafanikio ya Mubarak ya enzi ya vita.
Rais wa sasa wa Misri Abdel Fatah al-Sissi, alihudhuria kwa muda mfupi, na kutoa salamu zake ra rambirambi kwa kupeana mkono na watoto wawili wa Mubarak, Alaa na Gamal na mkewe Suzanne.
Mwili wa Mubarak umezikwa kwenye eneo la makaburi ya familia yake la Heliopolis viungani mwa mji mkuu wa Cairo
Social Plugin