Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amefika ofisi za makao makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma kuhojiwa.
Jana Ijumaa Januari 31, 2020 Takukuru alihojiwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola, Meja Jenerali Jacob Kingu (alikuwa katibu mkuu) pamoja na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.
Viongozi hao wanahojiwa baada ya agizo la Rais wa Tanzania, John Magufuli kuitaka Takukuru kuwahoji wale wote waliohusika na mkataba aliodai una harufu ya ufisadi ulioingiwa kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kampuni moja ya Romania kununua vifaa mbalimbali vya jeshi hilo.
Social Plugin