Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipeana mkono na Kiongozi wa Ujumbe
kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw.
Sikhumbuzo Dlamini, baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao, Jijini
Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na
Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),
ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (kushoto), wakiwa katika Mkutano
katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea umuhimu wa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kutathmini ukuaji wa
uchumi, wakati wa Mkutano wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
za Kusini mwa Afrika (SADC), ulioongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini
kutoka Eswatini, Jijini Dodoma
Kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini
akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb), (hayupo pichani), ambapo aliipongeza Serikali kwa kazi
nzuri inayofanya katika kukuza uchumi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akimuongoza mgeni wake ambaye ni
kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini, ulipotembelea katika Ofisi za
Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), akiwa katika picha ya pamoja
na Ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),
uliongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (wa nne kulia), pamoja na viongozi
wa Wizara hiyo na wajumbe kutoka SADC, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Ujumbe kutoka Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw.
Sikhumbuzo Dlamini (katikati), wakifuatilia mada zilizokuwa
zikiwasilishwa katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe
wa Mkutano wakifuatilia mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Ujumbe kutoka Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw.
Sikhumbuzo Dlamini (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dodoma.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dodoma)
Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo
chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
zinatakiwa kujitazama na kushauriana kuhusu mwenendo wao wa uchumi
badala ya kuyaachia Mashirika ya Kimataifa pekee.
Rai hiyo
imetolewa Jijini Dodoma wakati wa Mkutano kati yake na Ujumbe wa SADC
unaoongozwa na Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambao umetembelea nchini kwa ajili
ya Mpango wa kujitathmini kiuchumi kwa mwaka wa Fedha 2019/20.
Dkt. Mpango
alisema kuwa nchi za Afrika zimezoea kuona Benki ya Dunia (WB) na
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) au kuja kuangalia namna gani Uchumi
unavyoendelea ili hali Afrika hasa nchi za SADC zina fursa pia ya
kutembeleana na kushaurina namna bora ya kuendeleza uchumi na
kuwahudumia wananchi ikizingatiwa kuwa nchi hizo zinafahamiana vizuri.
“Madhumuni ya
ujumbe wa SADC kutembelea nchini ni kuangalia hali ya ukuaji wa uchumi,
ubadilishanaji wa fedha za kigeni, mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi
na kushauri mahali ambapo Tanzania haijafanya vizuri au kutumia fursa
ipasavyo’’, alieleza Dkt. Mpango.
Alisema kuwa nchi
za SADC zilikubaliana kuchagua ujumbe ambao utakuja nchini kufuatilia
namna uchumi Mkuu unavyoendelea, hivyo ametumia fursa hiyo kueleza
utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Umeme wa Maporomoko ya Mto
Rufiji, ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) na miundombinu
mingine ya barabara.
Kwa upande wake
Kiongozi wa Ujumbe wa SADC, Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambaye pia ni Meneja
wa Sera za Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Eswatini, ameipongez
Tanzania kwa maendeleo makubwa iliyofikia baada ya kujionea miradi
mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Reli, miradi ya maji ambayo
itasaidia ukuaji wa uchumi Uchumi Mkubwa na kuiwezesha kufikia Malengo
ya Maendeleo endelevu.
Social Plugin