Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza muda wa uandikishaji katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa ya Dar es Salaam.
Muda uliongezwa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura ni siku tatu ambapo zoezi hilo litaitimishwa Februari 23, 2020.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchanguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt Wilson Charles amesema kuwa kusogezwa kwa zoezi hilo kumetokana na maombi mbalimbali katika vituo vya uandikishaji.
Dkt.Charles amesema baada ya maombi hayo walifanya kikao cha Februari 19 kwa ajili ya kutathmini zoezi hilo na kuamua kuongeza muda wa kujiandikisha. Amesema vituo vyote vitafunguliwa kama kawaida kuanzia saa mbili hadi saa 12 jioni.
Social Plugin