Wabunge nchini Burkina Faso wamepitisha kwa kauli moja muswada utakaowezesha raia wa kupewa silaha ili kupambana na makundi yenye ya waasi.
Muswada huo ambao sasa unasubiri kutiwa saini na Rais unalengo la kupunguza mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wenye uhusiano na makundi ya al-Qaeda na Islamic State.
Muswada hu unasema kuwa, uwezo wa jeshi wa kupambana na wanamgambo na makundi ya wabeba silaha hautoshi kutokana na idadi yao kuwa ndogo na kuna ukosefu wa mafunzo yanayofaa.
Burkina Faso, kama zilivyo nchi jirani za Mali na Niger imekuwa ikiandamwa na mashambulio ya kigaidi ya mara kwa mara, ambapo tangu mwaka 2015 hadi sasa watu 750 wameshauawa na wengine zaidi ya 560,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulio hayo.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa katika eneo la magharibi mwa Afrika katika mwaka uliomalizika wa 2019 yameua raia elfu nne wa nchi za eneo hilo.
Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na baadhi ya wadau wa haki za binadamu kwa madai kuwa ni hatari kwa usalama wa raia.
Social Plugin