Raia wa Uganda wanaoishi kaskazini mwa wilaya ya Kitgum wanakula nzige wa jangwani ambao wameharibu mimea yao kulingana na kituo cha habari cha Uganda radio Nnetwork URN.
Hatua hiyo inajiri baada ya ripoti nyingine kwamba raia wa Somali pia wamekuwa wakibadilisha janga hilo la uvamizi wa nzige na kuwafanya kitowe wadudu hao
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinasema kwamba raia wa mji wa Adado katikati mwa Somalia wamekuwa wakiwakamata wadudu hao na kuwafanya kitoweo.
Raia mmoja amesema kwamba wadudu hao ni watamu kushinda samaki.
Mwingine amesema kwamba anaamini kwamba wadudu hao wana manufaa ya kimatibabu na kwamba anawafanya kitoweo kwa matumaini ya kupunguza uchungu uliopo mgongoni mwake pamoja na shinikizo la damu.
Baadhi ya wakazi wameitaka migahawa kuanzisha chakula cha nzige hao.
Uvamizi wa nzige hao katika baadhi ya maeneo mnchini Somalia na Ethiopia umeharibu mimea na kutishia baa la njaa katika eneo hilo kulingana na shirika la chakula duniani FAO.
-BBC
Social Plugin