Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa msimamo wa serikali juu ya mgogoro baina ya Magere Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu mara baada ya kusikiliza na kujadili hoja za pande zote. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Simon Msanjila.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza jambo wakati wa kikao kilichokua kikijadili mgogoro baina ya Magere Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara Jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo wakati wa kikao kilichokua kikijadili mgogoro baina ya Magere Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara Jijini Dodoma
Mlalamikaji Magere Mang’era akiwasilisha lalamiko lake mbele ya viongozi waandamizi wa wizara alipofika katika kikao hicho ili kutatua mgogoro baina yake na Joseph Ocheng Ndugu
Joseph Ocheng Ndugu akionesha mipaka ya eneo lenye mgogoro baina yake na Magere Mang’era wakati wa kikao kilichofanyika jana tarehe 12/02/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Madini jijini Dodoma
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na mmoja wa wajumbe wakisubiri kuanza kwa kikao cha kutatua mgogoro baina ya Magere Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Madini jijini Dodoma
Waziri wa Madini, Doto Biteko akimwonesha
mlalamikiwa moja ya nyaraka yenye udhibitisho katika mgogoro baina ya Magere
Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu wakati wa kikao cha kutatua mgogoro huo.
Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na kulia kwake ni
Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Simon Msanjila.
Katibu wa mgodi wa Irasanilo Samuel Matara alipokuwa akizungumzia historia ya mgogoro baina ya Magere Mang’era na Joseph Ocheng Ndugu mara baada ya kupewa nafasi ya kuzungumzia mgogoro huo na kutoa maoni yake
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Nyaisara Mgaya
akielezea hatua zilizofikiwa katika kutatua mgogoro wa Irasanilo katika kikao
kilichohusisha Viongozi Waandamizi wa Wizara, kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Wizara jijini Dodoma tarehe 12/ 02/2020
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko amewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini nchini kutumia Ofisi za Wizara katika kufikisha changamoto zao badala ya kufikisha kero zao kwa viongozi wengine wa nchi na serikali wasio na dhamana ya kusimamia Sekta ya Madini, kwani kufanya hivyo ni kuchelewesha utatuzi wa kero zinazowakabili.
Waziri
Biteko aliyasema hayo Februari 12 mwaka huu wakati wa kikao
kilicholenga kumaliza mgogoro baina ya wachimbaji wadogo Magere Mang’era na
Joseph Ocheng Ndugu waliokuwa wakigombea umiliki wa eneo la mita 23 lililopo
katika leseni ya Irasamilo Gold Mine iliyopo Buhemba Wilaya Butiama
mkoani Mara.
Pamoja na hayo, Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wa Mkoa wa
Mara kupunguza migogoro na kuwaeleza wizara yake inatamani kukutana nao kwa nia njema na si kwa
lengo la kujadili na kutatua migogoro ambayo inarudisha nyuma maendeleo yao na
nchi kwa ujumla.
“Wizara inashughulika na sekta ya madini nchi nzima, kama
kila mchimbaji atataka kuleta malalamiko yake ofisini kwa waziri basi kazi
hazitafanyika.” Tungefurahi kukutana nanyi kuwaeleza vitu mnavyotakiwa
kuviboresha ili kuongeza mapato ni si kutatua migogoro, Biteko alisisitiza.
Aidha,
Biteko ameutaka uongozi wa mgodi na uongozi wa wachimbaji wadogo ngazi za
wilaya na mkoa (Marema) kuhakikisha kwamba amani inatawala kwa wachimbaji na
kuwafanya wachimbaji wachimbe na kuzalisha kuliko kutengeneza migogoro
isiyoisha inayochangia katika kurudisha nyuma maendeleo yao. “Wanaotafuta pesa
hawatumii muda mwingi kugombana”, amesisitiza Biteko.
Baada ya kufikia hatma ya mgogoro huo na kumtaka Afisa Madini
Mkazi Nyaisara Mgaya kusimamia haki katika eneo hilo kama kikao kilivyoafiki
kuwa mwenye haki ya kupewa eneo hilo ni Magere Mang’era, Biteko aliwataka
wajumbe walioshiriki kikao hicho kurudi Mara na kuendelea na shughuli za
uzalishaji huku wakitunza amani na ushirikiano miongoni mwao.
Aidha, aliwataka kumtumia Afisa Madini Mkazi aliyepo katika
eneo hilo kama mlezi lakini pia alimtaka Afisa huyo kuishi na wachimbaji hao
vizuri na kudumisha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila
siku.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliutaka
uongozi wa Wachimbaji wadogo wa madini (Marema) kusimamia haki kwa wananchi
waliowapa dhamana ya kuwaongoza ili kupunguza migogoro inayojitokeza mara
kwa mara.
"Mkoa
wa Mara umejaliwa kuwa na rasilimali madini nyingi, msigeuze neema hiyo kuwa
chanzo cha migogoro na kutishiana maisha", alisema Naibu Waziri
Nyongo.
Aliendelea
kusema Neema ya Rasilimali madini
inapogeuka na kuwa chanzo cha matatizo na
migogoro inahuzunisha.
Aidha,
Nyongo alizitaka pande zote kukubaliana na matokeo na kuwa maamuzi yaliyofikiwa
yasiwe chanzo cha mgogoro mwingine, "naomba kabisa amani itawale".
Naye,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila aliwataka wajumbe wa
mkutano huo kuheshimu maamuzi ya Serikali na kutokuifanya serikali
kutumia gharama kubwa katika kutatua migogoro ya wachimbaji badala yake muda
unaotumika kutatua migogoro utumike kukusanya mapato ya serikali.
“Tumeweka ofisi za madini mikoani ili kupunguza matatizo
madogo madogo kuletwa wizarani hivyo mzitumie ofisi hizo na kuamini maamuzi
yanayotolewa na viongozi katika mikoa yenu yanakuwa Baraka zetu”. Msanjila alisisitiza.
Prof. Msanjila aliwahakikishia wajumbe kuwa maamuzi
yaliyofikiwa na Wizara ni sahihi na ya mwisho na kubainisha kuwa endapo
hawakubaliani na maamuzi hayo basi wasingefika katika kikao hicho.
Profesa
Msanjila alisisitiza kuwa, mlango sahihi wa kutatua migogoro katika sekta ya
madini ni Wizara ya Madini vinginevyo ni kupoteza muda na rasilimali.
Kwa
upande wa wajumbe walioshiriki kikao hicho wengi walikiri kuwa mwenye haki ya
kupewa eneo lililokuwa na mgogoro ni Magere Mang’era na kwa Mamlaka aliyonayo
Waziri aliamuru eneo lenye mgogoro apewe mlalamikaji na kuhitimisha mjadala juu
ya mgogoro huo.
Social Plugin