Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma.
Na. Josephine
Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imezitaka timu zote za mpira zinazoajiri
makocha na wachezaji kutoka nje ya nchi kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao wanaotakiwa kulipa kodi.
Hayo
yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Selemani Nkamia, aliyetaka kujua Serikali inatambuaje Kocha au Mchezaji wa Nje
aliyelipa na asiyelipa kodi kwa kuwa malipo yao hufanywa kiholela kwa kuwa
hakuna mfumo rasmi.
Dkt. Kijaji alisema kuwa Kila
mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira ndani ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na kipato chake.
“Kila mgeni akifikisha miezi 6 anahesabika ni mkazi (local resident) na anapaswa kulipa kodi,
ni jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani analipwa nini ili kodi zote stahili
ziweze kulipwa kwa mujibu wa sheria”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa ulipaji wa kodi ya ajira ni kwa mujibu wa
Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 na ni jukumu la mwajiri kwenda kutoa
taarifa kwenye Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao
wanaotakiwa kulipa kodi hiyo.
Dkt. Kijaji alisema kuwa katika mwaka wa fedha
2017/2018 jumla ya Sh. milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya
ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.
Social Plugin