Mabingwa watetezi, Simba SC wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Sixtus Sabilo alianza kuifungia Polisi dakika ya 23, kabla ya Nahodha John Raphael Bocco kuisawazishia Simba dakika ya 57 na Ibrahim Ajibu kufunga la ushindi dakika ya 90 na ushei.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 19, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya Azam FC wanaofuatia nafasi ya pili, ingawa wana mechi moja mkononi.
Social Plugin