BARABARA ZILIZOHARIBIWA NA MVUA UKEREWE KUANZA KUTENGENEZWA



Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na barabara zinazotengenezwa na Tarura.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala Za Mikoana serikali za Mitaa Josephat Kandege akiwa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Maendelea pamoja na barabara zinazotengenezwa na Tarura.


Na Geofrey A. Kazaula - UKEREWE
Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Mhe, Josephat Kandege ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kufanya ukarabati kwa barabara zilizoharibiwa na mvua Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza.


Ameyasema hayo alipotembelea barabara hizo ili kujionea hali halisi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza.

‘‘TARURA mnafanya kazi nzuri ila nitoe wito kuwa pale mnapo endelea na ujenzi wa barabara hizi mjitahidi kuangalia maeneo korofi yaliyoharibiwa sana ndo mkaanze nayo ili wananchi hawa wapate huduma’’, amesema kiongozi huyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa barabara za Vijijini kutoka TARURA Mhandisi Abdul Digaga amesema kuwa tayari kuna fedha kiasi cha Sh 50 Millioni zilizoletwa Ukerewe kwaajili ya kufanya matengenezo ya barabara hasa kwa maeneo yaliyoharibiwa na mvua ambapo Meneja wa TARURA Katika Halmashauri ya Ukerewe Mhandisi Reuben Muyungi amekiri kupokea fedha hizo na kwamba Mkandarasi tayari amepatikana na kazi itaanza wiki ijayo.

Naye Mbunge wa Ukerewe Mhe, Joseph Mkudi amesema kuwa kazi inayofanwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini - TARURA ni kubwa na kusema kuwa kuna haja ya Serikali kuongeza bajeti ya Wakala huo ili uweze kutekeleza majukumu yake kwa urahisi kwani kazi inayofanyika inaonekana licha ya ufinyu wa bajeti.

‘‘Mimi kama mbunge nitaendelea kujenga hoja kwa Serikali ili iongeze bajeti ya TARURA barabara zetu ziweze kutengenezwa kwa urahisi na kuwapatia wananchi wetu huduma’’ amesema Mkudi.

Mmoja wa wananchi Katika Kata ya Ukerewe Ndg,Nesphory Kangi amesema kuwa TARURA inasaidia sana kuwajengea barabara na miundombinu miingine na na kwamba kuna upungufu wa barabara za lami ambapo ameomba Serikali iwaongezee barabara hizo.

Miradi mingine iliyokaguliwa na Mhe, Kandege ni pamoja na Kituo cha Afya cha Busya -Ukara, Vikundi vya akina mama vinavyokopeshwa na Halmashauri kupitia mgawanyo wa asilimia kumi ya mapato ya ndani pamoja Ujenzi wa Vyumba vya madarasa vine na Ofisi moja ya Walimu Katika shule ya Msingi Murunsuli ambapo pia ameweka jiwe la Msingi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post