SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAFUGAJI WA SAMAKI KUENDELEA KUBORESHA ZAIDI MAZINGIRA BORA YA UFUGAJI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewahakikishia wafugaji wa samaki nchini kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwawezesha wafugaji kufuga samaki. 

Mhe. Ulega ameyasema hayo Februari 26,2020 kwenye Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali, Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga uliofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki. 

Mhe. Ulega amesema mabwawa ya samaki yameongezeka kutokana na jitihada zilizopo na kueleza namna serikali inavyoendelea kudhibiti uvuvi haramu Baharini na kwenye Maziwa. 

“Kabla ya serikali ya Awamu ya Tano katika Ziwa Victoria tulikuwa na vizimba vya ufugaji wa samaki visivyozidi 50 hivi leo tuna vizimba zaidi ya 400 vya ufugaji wa samaki maana yake mwitikio ni mkubwa sana baada ya kufanyika jitihada za makusudi kwamba haturuhusu samaki kuingia Tanzania kwa sababu sisi tuna uwezo wa kufuga na wenyewe kuweza kutumia.” Ameeleza

“Mwanzo tulikuwa na tatizo la bina lakini hivi sasa tupo kwenye hatua nzuri bima kwenye mifugo na uvuvi ili upatikanaje wa fedha kwenye eneo hili uwe wa uhakika kwa wafanyabiashara",Amesema. 

Amesema kwa upande wa Ziwa Victoria, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepata fedha nyingi kwa watu wenye lengo la kufuga samaki na kwa kuwa soko lipo la uhakika sasa ndiyo maana watu wengi wameingia katika ufugaji na uvuvi.

“Tumeweka Mazingira mazuri ya kuhakikisha kwamba Watanzania wanaoingia kwenye biashara za mifugo na uvuvi wapate soko. Mwanzo tulikuwa tunaagiza nyama nyingi kutoka nje ya mipaka yetu lakini serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli imefanya kazi kubwa na sasa hatuingizi nyama kutoka nje isipokuwa kwa kibali maalumu tu”,amesema Mhe. Ulega. 

Mhe. Ulega amesema fursa kubwa iliyopo sasa ni biashara ya kunenepesha mifugo na kupeleka kwenye viwanda vya nyama vilivyoanzishwa na vinavyotarajiwa kuanzishwa. 

“Hivi viwanda tunavyovianzisha hakika vitahitaji malighafi, ni lazima iwe malighafi ya uhakika kwa hiyo biashara iliyo nzuri sana sasa hivi ni biashara ya kunenepesha mifugo yetu. Kuwa na uhakika unapeleka viwandani mifugo iliyotunzwa na kunenepeshwa vizuri. Nakuhakikishia kwamba uchumi wako utakuwa kwa haraka sana,utapata pesa nyingi sana.” Amesema Mhe. Ulega. 

Amesema serikali imeshawishi taasisi za fedha na zimekubali kuingia kwenye biashara za kunenepesha mifugo na uvuvi na kubainisha kuwa jambo hilo linahitaji ushirikiano kati ya serikali na nyinyi wadau kwa ujumla. 

“Kwa upande wa ngozi bado tuna changamoto kubwa ya ngozi zetu, jitihada kubwa zimefanyika kuhakikisha tunapata suluhu ya hili jambo la ngozi. Tunahakikisha viwanda vyetu vinaanza uzalishaji, kama tulivyofanya katika uvuvi.” Ameongeza. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali itaendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara na kuwakumbusha kufuata sheria na kanuni zilizopo katika biashara na uwekezaji na wanapokuwa na migogoro wasisite kuwasiliana na serikali ili kuitatua.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga Februari 26,2020 kwenye ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiwahamasisha wafanyabiashara kuanzisha biashara ya kunenepesha mifugo na kupeleka kwenye viwanda vya nyama vilivyoanzishwa na vinavyotarajiwa kuanzishwa ili wapate pesa.

Wafanyabiashara, Wawekezaji na wadau mbalimbali wakimsikiza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega.

 Wafanyabiashara, Wawekezaji na wadau mbalimbali wakimsikiza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga (kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akizungumza kwenye Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akizungumza kwenye Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Mhe. Jumanne Kishimba na Mbunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele (katikati). Kushoto ni Mwenyekiti wa TCCIA,Dkt. Meshack Kulwa.
 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia : WAZIRI KAIRUKI AONGOZA MKUTANO MKUBWA WA MASHAURINO KATI YA SERIKALI,WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI MKOA WA SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post