Urusi imesema leo kuwa madai ya kitengo cha ujasusi cha Marekani kwamba nchi hiyo inaingilia kampeni za uchaguzi za mwaka 2020 na kujaribu kuongeza nafasi ya kuchaguliwa kwa mara nyingine kwa Rais Donald Trump ni uongo mtupu.
Mtu aliye na taarifa za karibu kuhusiana na suala hilo amesema maafisa wa ujasusi wa Marekani waliwaambia wabunge juma lililopita kwamba Urusi inaingilia kati kampeni ikiwa inalenga kutia mashaka kuaminika kwa uchaguzi huo ili kuiweka nafasi ya Trump kuchaguliwa tena kuwa juu.
Na sasa msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema yote ni uongo na wana wasiwasi kwamba uvumi huo utaenea kadri uchaguzi unapokaribia.
Social Plugin