Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema wanaejshi wa Uturuki wataendelea kuyajibu mashambulizi ya serikali ya Syria, wakati pande hizo mbili zikifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kaskazini mwa Syria.
Maafisa wa Uturuki walisema jana kuwa wanajeshi 101 wa serikali ya Syria waliuawa kufuatia mauaji ya Waturuki watano katika eneo la Idlib - ngome ya mwisho ya waasi.
Idadi hiyo hata hivyo haijathibitishwa na chombo huru.
Wakati huo huo, waasi nchini Syria wameiangusha helikopta ya serikali leo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, ambako wanajeshi wa serikali wanaendeleza mashambulizi katika ngome ya mwisho ya waasi.
Kudunguliwa kwa helikopta hiyo kumekuja wakati wanajeshi wa serikali wakikaribia kuikamata sehemu ya mwisho inayodhibitiwa na waasi ya barabara kuu muhimu inayounganisha kusini na kaskazini mwa Syria.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa vikosi vya Rais Bashar al-Assad kuchukua udhibiti kamili wa barabara hiyo tangu mwaka wa 2012.
Social Plugin