Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya Watu 20 waliofariki dunia Jumamosi Februari 1,2020 katika ibada ya mahuburi wakati wa harakati za kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' katika Viwanja vya Majengo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kufuatia taarifa kwa umma, Rais ametuma salamu hizo leo Jumapili, Februari 2, 2020 kufuatia ajali hiyo iliyotokea jana usiku baada ya kukanyagana katika harakati za kutaka kukanyaga mafuta ya upako kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwaiposa lililofanyika uwanja wa Majengo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pia amewaagiza wakuu wa mikoa ambao mikoa yao imekumbwa na mafuriko na kuathiri familia zaidi ya 20 waliopoteza maisha kutokana na madhara ya mvua kubwa zinazonyesha mkoani Lindi na mikoa mingine hapa nchini.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa watu 20 waliofariki dunia, walikuwa miongoni mwa watu waliokusanyika katika viwanja vya hivyo kuhudhuria ibada iliyoongozwa na mtume huyo na wamefariki dunia baada ya kukanyagwa na wenzao wakati wakitoka katika lango moja waliloelekezwa kupita ili kukanyaga mafuta ya upako huku wengine 16 wakijeruhiwa.
Watu wengine zaidi ya 20 wamefariki dunia Mkoani Lindi na katika mikoa mingine hapa nchini ambayo imekumbwa na madhara yatokanayo na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.
Rais ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya vifo vya Watanzania waliopoteza maisha katika matukio hayo na amewaombea marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka na kurejea katika majukumu yao.
Social Plugin